2 Chronicles 36:11-12

Mfalme Sedekia Wa Yuda

(2 Wafalme 24:18-20; Yeremia 52:1-3)

11 aSedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. 12 bAlifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la Bwana.
Copyright information for SwhNEN